Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Mpango ametoa msisitizo kwa wakulima wa zao la parachichi mkoani Njombe kuuza parachichi zilizo komaa.
Mhe Dkt Mpango ametoa msisitizo huo Julai 20,2023 Mjini Makambako alipo simama kusalimia wananchi wa mkoa wa Njombe.
Amesema wakulima wanao wajibu wa kulinda soko la parachichi ambayo ni dhahabu ya kijani kwa kuacha kuuza matunda ambayo hayaja komaa vizuri.
“Ninajua wanawashawishi lakini hawa watu siyo wazuri wanatuharibia ,wanapeleka huko kwenye masoko ulaya na parachichi yetu inaonekana haifai.”
Aidha ametoa maelekezo kwa waziri wa kilimo Mhe Hussein Bashe kupitia wizara ,viongozi na wataalamu mbalimbali Mkoani Njombe kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wakulima juu ya hasara zitokanazo na uuzaji wa parachichi ambazo hazijakomaa,lengo ikiwa nikulinda soko la parachichi.
Kuhusu suala la uuzaji wa mazao ya kilimo kwa mtindo wa rumbesa ,Dkt Mpango ameikumbusha wizara husika kwenda kusimamia na kuzingatia sheria iliyowekwa yakuzingatia vipimo sahihi kwenye ununuzi wa bidhaa za kilimo.
“Wananchi hawa wanafanya juhudi kubwa mno ni lazima tuwalinde wapate haki ya jasho lao na kwa hili nitaendelea kupiga kelele,tuache hii inawaumiza sana tutumie vipimo sahihi”
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais Mhe Dkt Philip Mpango,amewaomba viongozi wa dini pamoja na viongozi wengine kuendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa lishe bora hasa kwa watoto ili kuweza kuandaa kizazi bora cha baadaye.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe