Mkuu wa idara ya Elimu Msingi Halmashauri ya Mji Njombe Bi. Shida Kiaramba ametoa wito kwa shule zote za msingi Halmashauri ya Mji Njombe kuhakikisha zinakuwa na programu za michezo kwa wanafunzi ili kuwajenga kiafya na kiakili.
Ametoa rai hiyo Oktoba,15, 2023 akiwa ni mgeni rasmi kwenye fainali za mashindano ya Mpete Diwani Cup kwa Shule za Msingi zilizopo Kata ya Utalingolo Halmashauri ya Mji Njombe.
"Nitoe wito kwa shule nyingine zilizopo halmashauri ya mji Njombe kutenga muda wa michezo ili kuwawezesha watoto kujenga afya zao na kiakili hasa wanapokuwa wanafundishwa darasani."
Aidha Bi.Shida kiaramba amempongeza Mhe.Erasto Mpete mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe na diwani wa kata hiyo kwa kuanzisha mashindano hayo ambayo yanatasaidia kukuza vipaji vya watotom
"tumewaona watoto wakicheza ,wanaonesha nyuso za furaha , tunashukuru sana Mhe, Erasto Mpete hakika huu ni mchango mkubwa sana ambao umeuleta kwa halmashauri yetu ,naimani mashindano haya tutawatoa watoto wengi wa Umitashumta kwenye kata ya Utalingolo" Alisema Bi.shida kiaramba.
Kwa upande wake Mhe,Erasto Mpete Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe na Mkurugenzi wa Mpete Agrovert Center amesema wemeweza kufanikisa mashindano hayo kwa kutoa vifaa vya michezo ,kwa shule zote za kata ya Utalingolo huku akitoa rai kwa shule zote za Halmashauri ya MjI Njombe kuhakikisha wanafunzi asubuhi wanakimbia mchakamchaka kulingana na uwezo wa umri wao.
“Kwa kushirikiana na watumishi,na viongozi wa kata tuliona michezo imeshuka kwa pamoja tumehakikisha kwamba shule zetu ndani ya kata ya Utalingolo tunadumisha michezo. Alisema Mhe Mpete.
Shule ya Msingi Utalingolo ilingara kwenye mashindano hayo ya Mpete Diwani Cup 2023 kwa Shule za Msingi kata ya Utalingolo, nakujinyakulia kombe kwenye mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete (netball) kwa wasichana.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe