Oktoba 7, 2024, Halmashauri ya Mji Njombe imesaini mikataba na kampuni ya Ingenuity Works Limited na Hamerkop International Limited kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule na huduma za afya.
Hafla ya kusaini mikataba hiyo ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe, Mhe. Erasto Mpete, ambaye alizitaka kampuni hizo kutekeleza miradi kwa ubora na ufanisi ili kukidhi matarajio ya wananchi.
Mhe. Mpete alisisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa akifanya jitihada kubwa kuhakikisha fedha zinapatikana kwa ajili ya miradi hiyo,hivyo ni muhimu miradi hiyo itekelezwe kwa viwango vya juu na kwa kufuata miongozo sahihi.
Aliwataka wakandarasi hao kufanya kazi kwa unadhifu na ubora, tofauti na mafundi wengine.
Mikataba iliyosainiwa inajumuisha:
Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Wikichi, Kata ya Ramadhani kwa shilingi milioni 580,Ujenzi wa mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Matola kwa shilingi milioni 280 na Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Mji Njombe ( Kibena) kwa shilingi milioni 965.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe