Halmashauri ya Mji Njombe katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka wa fedha 2021/22 imepokea jumla ya Shilingi Milioni 167. 9 za mfuko wa jimbo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo jimboni.
Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Mhe. Deo Mwanyika alisema hayo mjini Njombe Aprili 20, 2024 wakati akiongea na makundi mbalimbali wakiwemo Wanyeviti wa vijiji na mitaa wa Halmashauri ya Mji Njombe, Watendaji wa Kata na Wataalamu wa Halmashauri.
Mhe. Mwanyika alisema, “fedha hizo zimeenda kutekeleza miradi maeneo mbalimbali kama Ununuzi wa mashine ya kutolea nakala (photocopy) katika shule ya Msingi Uliwa, ujenzi wa soko la kijiji cha Idunda, ufunguzi wa barabara kata ya Mjimwema na Njombe mjini” alisema na kuongeza kuwa, “mradi huu wa barabara utarahishisha mawasiliano na maeneo menginine ambayo yanauhitaji kwa wananchi.”
Katika hatua nyingine, Mbunge Mwanyika amegawa mifuko ya saruji 1,200 kwenye vijiji 20 na mitaa 3 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali katika mitaa na vijiji husika.
“Niwaombe wenyeviti tumieni mifuko hii ya saruji kwa ajili ya shughuli zilizokusudiwa,” alisema
Pia, Mhe. Mwanyika katika kipindi cha miaka mitatu ametoa shilingi Milioni 313,650,000/= fedha binafsi kwa ajili ya kuchangia maendeleo katika eneo la Njombe mjini.
Mwaka 2021 alitoa 103,576,000/=, 2022 alitoa 107,680,000/= na mwaka 2023 alitoa 102,400,000/=
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe. Erasto Mpete amemshukuru Mbunge kwa namna ambavyo anatekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi ambapo ametoa bure mitambo ya kusafisha barabara zenye changamoto.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe