Serikali imetenga shilingi milioni 75 kupitia Wakala wa Barabara za Mijini na Vijiji TARURA kwa ajili yakuweka taa za barabarani baada yakukamilika kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 1.57 Mabatini_Ramadhani iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 700.
Akizungumza Septemba 20,2024 wakati wa ziara ya Mhe.Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda Mkoani Njombe, Mhandisi Gerald Matindi amesema hakuna mkandarasi anayedai na barabara hiyo imekamilika kwa asilimia 100 ikiwa tayari imeanza kutumika.
Barabara ya Mabatini – Ramadhani ni kiunganishi kati ya kata ya Njombe Mjini na kata ya Ramadhani na kukamilika kwa barabara hiyo kumerahisisha usafiri kwa wakazi wa mji wa Njombe pamoja na usafishaji wa bidhaa na mazao mbalimbali ya kilimo.
Mradi huu umejengwa kwa awamu mbili awamu ya kwanza ikitumia fedha za mfuko wa jimbo na awamu ya pili ikijengwa kwa kutumia fedha za mfuko wa barabara.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe