Katibu tawala Mkoa wa Njombe Ndugu Judica Omary amekagua majengo yakutolea huduma yatakayofanyiwa ukarabati, pamoja na eneo litakalotumika kujenga majengo mapya yakutolea huduma katika hospitali ya Halmashauri ya Mji Njombe Kibena.
Katibu tawala ameitaka idara ya afya pamoja na uongozi wa hospitali kuhakikisha inasimamia vizuri fedha za mradi huo na kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwenye ubora unaotakiwa.
“Fanyeni ushindanishi wa mafundi,ulizeni gharama ya hivyo vitu kwa watu tofauti ili kupata gharama nafuu itakayotoa kazi bora na thamani ya fedha ionekane .”Alisema Bi Judica.
Majengo yatakayojengwa kwenye hospitali hiyo ni jengo la Kisasa la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD),jengo la kufulia na stoo ya Dawa (Pharmacy ).
Aidha ukarabati wa majengo utahusisha ukarabati wa wodi ya wanaume, wodi ya watoto, wodi ya daraja A na ukarabati wa jengo la wazazi (kuongeza huduma za uzazi kwa wateja maalum (VIP) delivery services.
Katika hatua nyingine ameishauri ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na ofisi za halmashauri kuona umuhimu wakujifunza ndani ya mkao kwa kufanya vikao vya idara nje ya halmashauri ili kuweza kuona namna wanavyotekeleza miradi ya maendeleo kwenye maeneo kwa lengo la kujifunza na kupata mawazo mapya.
Aidha Bi Judica alipata fursa yakuzungumza na akina mama waliokuwa wakipatiwa huduma kwenye jengo la mama na mtoto nakuwakumbusha, umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita, na kuendelea kunyonyesha mpaka mtoto atakapofikisha miaka miwili pamoja na lishe bora kwa mama mjamzito na watoto chini ya miaka mitano ,ili kupambana na utapiamlo na udumavu mkoani Njombe.
Halmasahuri ya Mji Njombe kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 imepokea fedha kutoka serikali kuu shilingi 900,000,000/= kwa ajili ya ukarabati wa Hospitali ya Kibena ambayo ni hospitali kongwe mjini Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe