Wajumbe wa kamati ya Fedha na Utawala Wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe.Filoteus Mligo ,Julai 18, 2024 wamefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 fedha kutoka Serikali kuu na Mapato ya ndani ya Halmashauri kwenye kata nne (4) za Halmashauri ya Mji Njombe.
Katika kata ya Utalingolo ulikaguliwa mradi wa ujenzi wa darasa moja(1) matundu nane (8) ya vyoo na nyumba ya mwalimu (2 in 1) katika Shule ya Sekondari Utalingolo kwa gharama ya Shilingi milioni 84.4.
Katika kata ya Ramadhani ulikaguliwa ujenzi wa vyumba vinne (4) vya madarasa,matundu nane (8 ) ya vyoo na ukamilishaji wa maabara mbili (2) katika shule ya Sekondari Kibena mradi wenye gharama ya shilingi milioni 129.4.
Kwa upande wa Kata ya Njombe Mjini ulikaguliwa mradi wa matengenezo ya barabara kwa kiwango cha lami mita 780 kutoka Glory hadi Mahakamani wenye gharama ya shilingi milioni 585 pamoja na mradi wa ujenzi wa ujenzi wa vyumba tisa (9) vya madarasa na matundu nane (16) katika shule ya Sekondari Mabatini na Mbeyela shilingi 253.8.
Na katika kata ya Mjimwema shilingi milioni 164.4 zinatekeleza ujenzi wa vyumba sita (6) vya madarasa na matundu nane(8) ya vyoo katika shule ya Sekondari Mpechi ,ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi shilingi milioni 62.5 na ujenzi wa vyumba sita (6) vya madarasa katika shule mpya ya Msingi Lunyanywi
mradi ulioanza kwa nguvu za wananchi Serikali imetoa shilingi milioni 50 ambazo zimekamisha vyumba viwili vya madarasa.
Kwa pamoja wajumbe wa kamati ya Fedha na Utawala Halmashauri ya Mji Njombe wameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ,kwa namna inavyoendelea kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia na kuhakikisha huduma za msingi zinasogezwa karibu na wananchi.
Aidha wametoa msisitizo kwa mhandisi wa Halmashauri kufanya usimamizi wa karibu kwa mafundi wote wanaotekeleza miradi hiyo ili iwe bora ikamilike kwa wakati na thamani ya fedha iliyotolewa ionekane.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe