Timu ya tathmini na ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe imefanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Njombe, yenye jumla ya thamani ya TZS bilioni 1.98.
Miradi hiyo inatekelezwa kupitia fedha kutoka:
* TASAF bilioni 1.01.
* BOOST (mpango wa elimu) milioni 620.4.
* Mapato ya Ndani milioni 267.9.
* Serikali Kuu milioni 88.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa shule mpya, mabweni na bwalo,Ujenzi na ukamilishaji wa zahanati,Nyumba za walimu na watumishi, Ukarabati wa miundombinu ya elimu na afya na Ununuzi wa vifaa tiba
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na :-
* Ujenzi wa shule mpya ya msingi eneo la Sekondari ya Mgola kwa gharama ya shilingi milioni 329.5.
* Ujenzi wa Bweni la S/S Anne Makinda kwa gharama ya sholingi milioni 138.1.
* Ujenzi wa Zahanati mpya ya mtaa wa Kambarage kwa gharama ya shilingi milioni 92.4.
* Ukarabati wa shule ya msingi Kambarage kwa gharama ya shilingi milioni 132.8
* Kuvisha Mitambo ya X-Ray kwenye Kituo cha Afya Muungano kwa gharama ya shilingi milioni 8.
* Ujenzi wa bwalo la chakula Shule ya Msingi Madobole kwa gharama ya sholingi milioni 153.1.
* Ujenzi wa uzio Zahanati ya Ikisa kwa shilingi milioni 92.4.
* Ujenzi wa nyumba ya watumishi Shule ya Msingi Iwungilo kwa shilingi milioni 82.2.
* Ujenzi wa zahanti ya kijiji cha Yakobi shilingi milioni 92.4.
* Ujenzi wa nyumba pacha zahanati ya Mgala kwa shilingi milioni 83.4.
* Ujenzi wa bweni S/S Kifanya kwa gharama ya shilingi milioni 138.1.
* Ujenzi wa bweni S/S Mgola kijiji cha Lugenge kwa gharama ya shilingi milioni 138.1.
* Ujenzi wa madarasa 3 na matundu 6 ya vyoo S/M Kibena shilingi milioni 88.
* Ukamilishaji wa bwalo 1 S/S Yakobi shilingi milioni 60.9.
* Ujenzi wa madarasa 2 S/M Selestine Kilasi shilingi milioni 50.
* Ukamilishaji wa nyumba ya mwalimu S/M Mapinduzi shilingi milioni 20.
* Ukamilishaji wa zahanati ya Itipula shilingi milioni 39.
* Ukamilishaji wa nyumba ya mwalimu S/M Mwembetogwa shilingi milioni 20.
* Ujenzi wa Madarasa 2 S/M Lufingu milioni 25.
* Ukamilishaji wa kituo cha afya Luponde shilingi milioni 30.
* Ukamilishaji wa nyumba ya Mtumishi wa afya zahanati ya Kitulila shilingi milioni 15.
* Ununuzi wa vifaa tiba katika zahanati ya Itipula milioni 33.
* Ujenzi wa bweni S/S Maheve milioni 15.
* Ujenzi wa bwalo S/S Utalingolo milioni 40.
* Ujenzi wa madarasa 2 na matundu 6 ya vyoo elimu ya awali S/M Nazareti Tsh. 70.1.
* Ujenzi wa madarasa 3 na matundu 6 ya vyoo S/M Kibena milioni 88.
Lengo kuu la ukaguzi huo ni kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ufanisi, kwa viwango vinavyotakiwa na kwa manufaa ya wananchi.
Timu hiyo imeridhishwa na hatua za utekelezaji na kutoa msisitizo kwa wasimamizi na mafundi ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe