Halmashauri Ya Mji Njombe imetoa misaada ya Kijamii yenye thamani ya Shilingi Milioni 5 Laki 4 kwa familia 16 za watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi na vituo viwili vya kulelea watoto yatima ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kusaidia watu wenye mahitaji maalumu.
“Sisi kila mwaka katika bajeti yetu Kitengo cha Ustawi Wa Jamii huwa tunaweka bajeti kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji kupitia mapato ya ndani. Kwa kipindi hiki tumetenga shilingi Milioni 5 na laki 4 na tutagawa kwa kaya 16 na vituo viwili vya watoto yatima ambazo zina hali mbaya sana” Alisema Mwenda Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe wakati wa Makabidhiano hayo.
Kwa upande wake Afisa Ustawi Halmashauri ya Mji Njombe amewaomba wadau wengine na jamii kwa ujumla kuguswa na kuendelea kuzisaida familia zenye uhitaji badala ya kusubiria Serikali pekee.
“Niwaombe wadau wengine na jamii kwa ujumla pale tunapoona kuna familia ipo katika mazingira hatarishi sisi tunaowazunguka tuwe wa kwanza kutoa misaada ili kuokoa hiyo familia,sio tu msaada wa kitu bali hata kuwaunganisha na watu wanaoweza kuwasaidia kwa sababu watoto sio wa serikali peke yake. Alisema Veronika Myango Afisa Ustawi Halmashauri ya Mji Njombe.
Wakizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo Nicholasias Mgaya naOliver Mtewele , amesema kuwa wanaishukuru Halmashauri kwa misaada hiyo kwani wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu na malazi yamekuwa tabu kwao.
Kwa wakati huo huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amemuagiza Mtendaji Wa Kijiji Cha Makanjaula kuhakikisha kuwa Wanashirikiana na Uongozi wa Kijiji kuona ni kwa namna gani wanaanza ujenzi wa nyumba ya kuishi ya Bibi Oliver Mtewele ambaye ni Mjane anayeishi na watoto wake watatu na anaishi katika nyumba ya nyasi kuwa na makazi bora na ya kudumu na amesema kuwa Halmashauri itagharamia ujenzi huo kwa kushirikiana na Serikali ya Kijiji na amesema kuwa zoezi hilo lianze mara moja.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe