Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ndugu Anthony Mtaka amewakaribisha watanzania wote wanaohitaji kufuga ngo'mbe wa maziwa, kufika kwenye Shamba la ngo'mbe kitulo lililopo wilaya ya makete mkoani Njombe kupata mitamba bora.
Mhe. Mtaka amesema hayo Oktoba 28,2023 wakati wa kukabidhi zawadi ya Mkoa kwa Mheshimiwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango, aliyekuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maonesho ya Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kitaifa Mkoani Njombe.
Amesema kuwa mkoa wa Njombe umetoa zawadi ya mitamba miwili yenye mimba kutoka Shamba la ngo'mbe kitulo ikiwa ni heshima kwa Mhe makamu wa Rais na habari njema kwa watanzania wote wafahamu kuwa, shamba la kitulo limefufuliwa na linazalisha mitamba bora yenye uwezo wa kutoa mpaka lita 30 za maziwa kwa siku.
"Mheshimiwa makamu wa Rais, kuna wakati wafugaji walilazimika kwenda mpaka Afrika kusini kununua ngo'mbe bora kutokana na shamba letu kuyumba, tunaamini kwa zawadi hii wewe mwenyewe utakuwa shahidi kwenye uzalishaji wa maziwa" Alisema Mhe. Mtaka.
Katibu tawala wa Mkoa wa Njombe Bi Judica Omari amekabidhi kamba zakufungia ngombe na mkoa utaratibu kusafirisha ngo'mbe hao hadi kufika nyumbani kwa Dkt Mpango.
Zawadi nyingine iliyokabidhiwa kwa Mheshimiwa makamu wa Rais Dkt Mpango ni Kiwanja chenye hati kilichopo Halmashauri ya Mji Njombe iliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe. Erasto Mpete, Pamoja miche ya karanga aina ya makademia.
Akizungumza baada yakukabidhiwa zawadi hizo Mheshimiwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango, ametoa shukrani kwa namna mkoa wa Njombe ulivyo mkarimu kwa kipindi chote alichofanya ziara mkoani Njombe, nakuhidi kurudi tena Njombe kutembelea maeneo ambayo hajafika.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe