Kuelekea Maadhimishonya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibari Halmashauri ya Mji Njombe Aprili 25,2024 imepanda miti 200 katika shule ya Sekondari Lunyanywi
Miti hiyo imepandwa na Wataalamu wa Vitengo mbalimbali kutoka Halmashauri ya Mji Njombe, Walimu pamoja na wanafunzi wa Shule hiyo
Katika zoezi hilo la Upandaji wa Miti Afisa Utamaduni Halmashauri ya Mji Njombe Clemence Manga amesema maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru yameambatana na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kupanda miti ya kivuli ambayo itasidia kwa wanafunzi katika usomaji pamoja na kutunza mazingira .
Aidha Afisa Utamaduni alisema kuwa Halmashauri pia katika kuenzi muungano huo imeanda mkesha wa maadhisho hayo katika viwanja vya stendi ya zamani Mjini Njombe ambapo kutakuwa nashughuli mbalimbali za waasisi wetu Mwalimu Julius Kambage Nyerere Rais wa Kwanza wa Tanganyika kabla Tanzania na Abed Amani Karume Rais wa kwanza wa Zanzibari .
Katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania yanaadhimishwa kwa kaulimbiu isemayo "TUMESHIKAMANA NA TUMEIMARIKA ,KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU"
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe