Katibu tawala Mkoa wa Njombe Bi.Judica Omari,Januari 08,2024 ametembelea shule ya mpya ya Sekondari Makowo iliyojengwa kwa gharama ya shilingi 583,000,000 kupitia mradi wa SEQUIP.
Akizungumza na wanafunzi ambao tayari wameripoti shuleni hapo amewataka kuitunza na kuitumia vizuri miundombinu mizuri ya shule hiyo na kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili waweze kutimiza malengo yao.
Aidha amewasisitiza kuepuka vishawishi vya namna yoyote ambavyo vinaweza kusababisha kukatisha ndoto zao.
Shule mpya ya Sekondari Makowo imepangiwa wanafunzi 95 na 27 tayari wameripoti Shuleni hapo kwa ajili yakuanza masomo. Shule hiyo inahudumia vijiji vitatu vilivyopo kwenye kata hiyo.Uwepo wa shule hiyo katika kata ya Makowo umesaidia kuwapunguzia wanafunzi umbali mrefu wakutembea kwenda kusoma katika shule ya Sekondari Matola iliyopo kata ya Matola.
Halmashauri ya Mji Njombe itoa shukrani na pongezi kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi ,hakika Serikali imewasikia wananchi wa Makowo na kuwafikia.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe