Kata ya Njombe Mjini Aprili 09,2024, imezindua mkakati wa kuimarisha lishe ndani ya kaya ili kutokomeza udumavu.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa mkakati huo Afisa Tarafa, Tarafa ya Njombe Mjini Ndugu Lilian Nyemele ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa amesema mpango huo utakwenda kuimarisha hali ya lishe na kufanya wananchi wa kata hiyo kuwa na afya bora.
Aidha ameeleza kuwa nguvu kubwa inahitajika kutokomeza udumavu hivyo ni muhimu kuwashirikisha wadau mbilimbali katika jamii, kuwajengea uwezo watoa huduma ngazi ya Jamii sambamba na kuendelea kutoa elimu ya lishe bora kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla.
Katika hatua nyingine amewaomba wenyeviti wa mitaa yote ya kata ya Njombe mjini kwa kushirikiana na watendaji kuhakikisha wanaimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao pamoja na kuendeleza shughuli za maendeleo katika mitaa ambayo wanatoka.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Ndg. Samson Medda amepongeza jitihada zinazofanywa na kata ya Njombe Mjini kuweka kipaumbele kwenye suala la lishe jambo ambalo linaenda kuimarisha afya za wototo pamoja na kuijenga jamii kuwa na kizazi kilicho bora ambacho hakitakuwa na udumavu.
Naye Alatanga Nyagawa Diwani wa Kata ya Njombe Mjini amewataka wenyeviti na viongozi wote wa kata kishirikiana na kuwa wamoja ili kutimiza lengo la kutokomeza udumavu ambao unatajwa kuwa ni asilimia 50 Mkoani Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe