Wakizungumza kwa wakati tofauti viongozi wa madhehebu ya dini na Kimila walioshiriki katika kongamano hilo wamesema kuwa Taifa la Tanzania hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Amani iliyopo katika Taifa letu ambayo ni nadra kupatikana katika mataifa mengine na kufanya Tanzania kuwa Nchi ya kipekee.
Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye amehamishiwa katika Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba ambaye ndiye mgeni rasmi katika kongamano hilo amesema kuwa dhumuni kubwa la kufanya kongamano hilo ni kutokana na sababu kuwa Serikali ya Tanzania ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kipindi kifupi imepokea fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mingi ya Maendeleo ambayo ipo iliyokamilika na mingine ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji jambo ambalo limepelekea Mkoa kuandaa maombi ya kumwombea Afya njema Mheshimiwa Rais lakini pia Taifa kuendelea kudumisha Amani,Umoja na Mshikamano
Mchungaji Richard Hananja @hananja.r amesema kuwa ili Taifa liweze kuendelea linahitaji amani na hivyo ni jukumu la Viongozi wa Dini ,Serikali, Wananchi kuombea Amani hiyo Kwa Mwenyezi Mungu ili aweze kuliepusha Taifa na majanga mbalimbali.
Shekhe Hilary Makarani maarufu Shekhe Kipozeo amesisitiza kuwa zipo Nchi chache duniani Tanzania ikiwa Miongoni ambazo Wanachi wake hawapendi mifarakano na wanapenda kuishi kwa Amani jambo ambalo Watanzania tunajivunia na kutupasa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi hiyo.
Wakitoa shuhuda zao katika ziara iliyofanyika siku Moja kabla ya Dua hiyo kwa kutembelea miradi inayotekelezwa katika Mkoa wa Njombe ikiwemo miradi ya barabara,soko kuu Njombe na kituo kipya Cha mabasi viongozi hao wadini wamesema kuwa Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na inayolenga kuwasaidia Wananchi wa Tanzania na hivyo Rais Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan anapaswa kuombewa na Taifa kuwekwa chini ya maombezi ili Maendeleo yanayokusudiwa na maono ya viongozi yaweze kuendelea kumfikia kila Mwananchi kwa Amani na utulivu."Binafsi sijawahi kuona barabara ya zege tangu kuzaliwa kwangu mpaka sasa ila nimekuja kuiona Njombe"alisema Hananja.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe