Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Anthony Mtaka Januari 27,2024 kwenye kilele cha kampeni ya kuongeza kasi yakupunguza udumavu Mkoani Njombe amekabidhi mpango mkakati wa miaka saba wakutokomeza udumavu Mkoani Njombe.
Amekabidhi mpango mkakati huo kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makambako Mheshimiwa Deo Sanga na Mheshimiwa waziri wa Katiba na sheria Dkt Pindi Chana.
Mpango mkakati huo wa miaka saba umekabidhiwa pia kwa viongozi wa dini , viongozi wa kimila pamoja na makundi mengine ili kila kila mmoja aweze kutambua anachotakiwa kutekeleza kwenye kampeni ya kuhamasisha lishe bora ili kuongeza kasi ya kupunguza udumavu Mkoani Njombe.
Kampeni ya Lishe ya Mwanao Mafanikio yake iliyozinduliwa Disemba 22,2023,ni kampeni endelevu ambayo inafadhiliwa na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo UNICEF na USAID kupitia mradi wa lishe mtambuka.
Kauli mbiu ya Kampeni hiyo inasema “Kujaza Tumbo sio Lishe,Jali unachomlisha.”
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe