• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe asaini Mikataba na Watendaji kupambana na Utapiamlo

Tarehe iliyowekwa: August 2nd, 2019

Akizungumza wakati wa  utiaji sahihi mikataba ya utendaji kazi na usimamizi wa shughuli za lishe kwa  Watendaji wa Kata, Mtaa  na Vijiji kutoka katika Kata 13 za Halmashauri ya Mji Njombe na Mkurugenzi wa Halmashauri, Bi. Illuminatha Mwenda Mkurugenzi wa Halmashauri amewataka  Watendaji hao kuhakikisha kuwa wanatekeleza yale yote yaliyopo kwenye mkataba huo ikiwa ni sambamba na kutoa elimu juu ya lishe na kuhimiza jamii  kulima bustani za mbogamboga, matunda na kula milo kamili ili kufikia adhma ya kuondokana na udumavu ambapo Mkoa wa Njombe unaongoza kwa asilimia 53.6.

“Akili inajengwa na Lishe bora, niwaombe Watendaji kuchukua hatua stahiki na kutekeleza wajibu. Kila mtu katika eneo lake ahakikishe kuwa lishe ni mojawapo ya agenda ya kudumu katika vikao vya Kamati ya Maendeleo ya Kata (KAMAKA).”Alisema Mwenda.

Akiwasilisha taarifa ya hali ya Utapiamlo na udumavu Mwakilishi wa Shirika la CUAMM ambao ni mmojawapo wa mdau wa mapambano dhidi ya Udumavu katika Mkoa wa Njombe, Neema Lazaro amesema kuwa  hali ya utapiamlo katika Mkoa wa Njombe ni kubwa  na kwa sasa hali ni mbaya zaidi kwa watoto chini ya miaka 5, wanawake wajawazito na akinamama wanaonyonyesha.

Neema amesema kuwa Utapiamlo unachangia maradhi, vifo na uchelewaji wa ukuaji wa mwili na maendeleo ya akili kwa watoto hali inayosababishwa na ulishaji duni,maradhi ya mara kwa mara na huduma hafifu za malezi na makuzi ya awali ya watoto wadogo.

Kwa upande wao Watendaji wa Kata ya Kifanya Ezekiel Busagala na Mtendaji wa Mtaa wa Ramadhani wao kwa upande wao wamesema kuwa watahakikisha kuwa utekelezaji wa Mkataba huo unaenda kufanyika ipasavyo na wataenda kutoa elimu kwa Wananchi ili kila Mwananchi aweze kuonjwa ni kwa namna gani swala la Utapiamlo na udumavu ni tatizo kubwa la linalohitaji jitihada za jamii katika kupambana nao.

Miongoni mwa majukumu ya msingi yaliyopo kwenye Mkataba huo kwa Watendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata ni kuhamasisha na kuhakikisha  wanashiriki kikamilifu katika kupanga  mpango kazi wa lishe, kuutekeleza, kuufuatilia na kuhakikisha vikao vyote vya kisheria vinajadili agenda ya Lishe.

Mkataba huo utakaodumu kwa muda wa miaka mitatu na kupimwa kasi ya utekelezaji wake kila  mwaka ni mojawapo ya afua zinazotumika katika kupambana na tatizo la Utapiamlo na Udumavu Katika Halmashauri ya Mji Njombe na Taifa kwa ujumla.






Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe