Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi.Kuruthum Sadick, Tarehe 11 Februari 2025 ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata ya Matola, Kifanya, Yakobi, Mjimwema, na Njombe Mjini. Katika ziara hiyo, aliambatana na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa zahanati ya Kambarage, mabweni ya shule za sekondari Matola na Kifanya, pamoja na nyumba ya mwalimu katika Shule ya Sekondari Yakobi, ambayo tayari imekamilika.
Akiwa katika ziara hiyo,alihimiza usimamizi wa karibu kwa mafundi ili kuhakikisha wanakamilisha miradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Halmashauri ya Mji Njombe inatoa shukrani kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi inayolenga kusogeza huduma karibu na wananchi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe