Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi.Kuruthum Sadick, Tarehe 11 Februari 2025 akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo, alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mpechi.
Aliwasisitiza wanafunzi hao kujituma kwenye masomo na kuzingatia utunzaji wa rasilimali wanazotumia ili ziweze kudumu na kutumiwa na vizazi vijavyo. Alikumbusha kuwa rasilimali hizo zikiwemo vyumba vya madarasa wanavyotumia vimejengwa kwa gharama kubwa, hivyo wanajukumu la kuhakikisha vinatunzwa ipasavyo wakishirikiana na waalimu wao.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe