Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka,Agosti 20,2024 alifanya ziara ya kukagua miundombinu mbalimbali iliyojengwa katika Shule mpya ya Msingi Umago iliyopo kata ya Uwemba kwa fedha za TASAF zaidi ya shilingi Milioni 600.
Miundombinu iliyokaguiwa inahusisha ujenzi wa nyumba ya mwalimu (2in 1),ujenzi wa Uzio ,ujenzi wa uwanja wa Michezo,vyumba vya madarasa ,matundu ya vyoo ,ofisi na bwalo la kulia chakula.
Pamoja na ukaguzi wa miundombinu hiyo Mhe.Mtaka alitumia fursa hiyo kusisitiza taaluma bora kwa kudhibiti utoro shuleni pamoja na kusisitiza wazazi kuhakikisha watoto wanavaa nguo nzito zitakazo wakinga na baridi kali ili kulinda afya zao.
Kukamilika kwa miradi wa ujenzi shule mpya ya Msingi Umago kumetatua changamoto kwa waafunzi haswa wanaotokea eneo la Majengo, mashariki A, maghahari A na eneo cha Mwanayago ambao walilazimika kutembea umbali mrefu kwenda shuleni jambo ambalo lilichangia utoro au kuacha masomo kwa baadhi ya wanafunzi.
Shule ya Msingi Umago ilianza kutoa huduma Januari 2022 na idadi ya wanafunzi waliopo shuleni sasa kuanzia darasa la awsali hadi darasa la saba ni wanafunzi 341.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe