Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa, ameunda Kamati maalum ya kuchunguza changamoto zinazokumba viwanda vya chai katika wilaya ya Njombe. Kamati hiyo inajumuisha wajumbe kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya pamoja na wadau wa zao la chai.
Uamuzi huo ulifikiwa Januari 23, 2025, katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Njombe, kufuatia malalamiko ya wakulima na wafanyakazi wa viwanda vya chai juu ya changamoto ya kutolipwa stahiki zao ikiwemo mishahara kwa wakati.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Kasongwa aliitaka Bodi ya chai kitaifa kutoa majibu yanayoeleweka kwa wakulima ili kukabiliana na hasara kubwa wanayoipata kupitia zao hilo. Aliongeza kuwa baadhi ya wakulima wameanza kufikiria kubadilisha matumizi ya mashamba yao kutokana na hali ngumu wanayokabiliana nayo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa wakulima wadogo wa chai nchini, Theofhord Ndunguru, alisema kuwa kuporomoka kwa zao la chai kunatokana na kushuka kwa kiwango cha unywaji wa chai duniani.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe