Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, leo amefanya ziara ya ukaguzi katika zahanati ya kijiji cha Mamongolo Halmashauri ya mji Njombe, kwa lengo la kujionea hali ya utoaji wa huduma za afya na changamoto zinazowakabili watumishi pamoja na wananchi wanaotegemea kituo hicho.
Akizungumza Julai 14, 2025 alipotembelea kituo hicho, Mkuu wa Wilaya ameridhishwa na juhudi zinazofanywa na watumishi wa kituo hicho za kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kutokana na zahanati mpya ambayo wameweza jengewa na serikali .
"Huduma za afya ni haki ya msingi kwa kila mwananchi ,Hatuwezi kuruhusu wananchi wetu wapate huduma duni kwasasa Serikali ya awamu ya sita inatilia mkazo maboresho ya huduma za afya vijijini, na sisi kama viongozi wa ngazi ya wilaya tutaendelea kusimamia hilo," alisema Mhe. Sweda.
Aidha, akiwa katika mradi huo wa zahanati Mpya ya kijiji hicho aliwataka viongozi wa kijiji kuendelea kushirikiana na wataalamu wa afya katika kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kujitokeza kupata huduma za afya, hususan kina mama wajawazito na watoto.
Ni tarehe 08 Juni 2025, ndoto za kuwa na zahanati ya kisasa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa kijiji cha Mamongolo ziliweza kutimia baada zahanati mpya yenye thamani ya zaidi ya milioni 146 kuzinduliwa na kuanza kufanya kazi katika kijiji hicho.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe