Mafunzo ya matumizi ya mfumo mpya wa kielektroni unaowezesha kufanya Usajili, Kuchakata Zabuni, Kusimamia Mikataba, Malipo na kununua kupitia Katalogi na Minada kimtandao (NeST) National e-Procurement System of Tanzania yamehitimishwa rasmi kwa Halmashauri sita za mkoa wa Njombe .
Septemba 08,2023 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Ndugu Ayubu Mndeme wakati akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe, ametoa rai kwa watumishi wote waliopatiwa mafunzo hayo kwenda kuwajibika vyema kwenye vituo vyao vya kazi pamoja na kuendelea kukumbushana taratibu za ununuzi.
Amesema mfumo huu unaenda kurahisisha utendaji kazi hivyo ni vyema kila mmoja kufuata utaratibu ulioelekezwa wakati wakuanza kutumia mfumo huo.
Katika hatua nyingine kaimu katibu tawala amewakumbusha watumishi walioshiriki mafunzo hayo kufanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ya utumishi umma.
“Rai yangu ni haya tujiepushe kufanya kazi kwa maslahi binafsi ,matokeo yake ni kuharibu kazi.”
Nao baadhi ya washiriki katika semina hiyo akiwemo Alfonce Bruno Afisa ununuzi Halmashauri ya mji Njombe ,Barnabas Lwakala Afisa ununuzi kutoka Halmashauri ya Mji wa Makambako pamoja Estar Magimila Kutoka Halmashauri ya wilya Njombe wamesema mfumo huo utaendaa kubadilisha na kurahisisha utendaji wa kazi tofauti na kupunguza matumizi ya karatasi kwenye zoezi la ushindani.
Serikali imeamua kutengeneza mfumo mpya baada ya mfumo uliokuwa ukitumika kwenye ununuzi katika sekta za umma TANEPS kubainika kuwa na changamoto,hivyo mfumo wa NeST unaenda kutatua changamoto hizo.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe