Wateja ambao hawajachukua fidia ya bima ya amana baada ya kufungwa kwa iliyokuwa Benki ya Wananchi ya Njombe (NJOCOBA) Januari 2018 ,wametakiwa kufika kwenye tawi la Benki ya Biashara ya taifa (TCB) zamani Benki ya Posta wakiwa na kitambulisho cha taifa (NIDA) ili kufanyiwa uhakiki kwa ajili ya kulipwa stahiki zao.
Wito huo umetolewa Mei 22,2024 na Joyce Shala Ofisa rasilimali watu mwandamizi wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kwenye semina ya siku moja kwa wadau wa Bodi hiyo kutoka Wilaya ya Njombe iliyolenga kutoa elimu kuhusu Bodi ya Bima ya Amana, majukumu yake na kutoa taarifa masuala ya ufilisi wa iliyokuwa Benki ya wananchi ya Njombe (NJOCOBA).
“Tunawaomba wale wote waliokuwa wateja wa NJOCOBA ambao hawajalipwa fidia wafike kwenye tawi lolote la Benki ya biashara ya taifa(TCB) ,watafanyiwa uhakiki na kupatiwa stahiki zao, NJOCOBA ilikuwa na jumla ya wateja 12,323 tayari tumelipa wateja 4,014 madai yao yaliyokuwa na thamani ya shilingi bilioni 1.2 sawa na asilimia 87 ya madai yote ,wateja ambao bado hawajalipwa madai yao ni 8,309 yenye thamani jumla ya shilingi milioni 189.”Alisema Bi.Joyce Shala.
Aidha Bi.Joyce amesema kuwa Bodi ya Bima ya Amana inaendelea na ufuatiliaji wa madeni ambayo hayajalipwa kutoka kwa waliokuwa wateja kwenye Benki ya wananchi ya Njombe (NJOCOBA).
“Tuna fanya kazi na mkusanya madeni anapita kwa wadaiwa,orodha tunayo na dhamana walizoweka tunayo na kwa takwimu za machi 2024 tunadai zaidi ya milioni 431 tunawakumbusha waweze kulipa madeni hayo.”Alisema
Bodi ya Bima ya Amana (DIB) tarehe 23 na 24 Mei 2024 itaendelea kutoa elimu kwa kuwatembelea wajasiriamali wadogowadogo walioko masokoni ,vituo vya pikipiki na maeneo mengine ndani ya Halmashauri tatu za wilaya ya Njombe ambazo ni Halmashauri ya Mji Njombe ,Halmashauri ya Mji Makambako na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe