Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Njombe Mhe. Erasto Mpete amewaomba wataalamu na waheshimiwa madiwani kwenda kuhamasisha suala la lishe katika mikutano ya kata (kamaka) pamoja na mikutano ya hadhara.
Mhe Mpete amesema hayo Aprili 30,2024 katika Mkutano wa Baraza la waheshimiwa madiwani robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo aliweza kuwaomba madiwani hao kuhakikisha wanakwenda kutilia mkazo kwenye suala la uduamvu kutokana na tawimu za mkoa wa Njombe kuwa katika hali ya kiwango cha juu ya watoto wenye udumavu kwa zaidi ya asilimia 50.4%.
Aidha katika mkutano huo Mhe. Mpete amesema kuelekea kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa ni muhimu madiwani na wenyeviti kwenda kuwaaambia wananchi kazi zilizofanywa na Serikali husani miradi ya maendeleo.
“Sasa hivi tunakwenda kwenye uchanguzi wa Serikali za mitaa kumekuwepo na baadhi ya watu kusahau miradi ambayo Serikali inatekeleza kwa kiwango kikubwa,niwaombe waheshimiwa madiwani twende tukawaambie wananchi miradi hiyo” Alisema.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe