Na Ichikael Malisa
Mradi wa kizazi hodari kanda ya kusini Septemba 29,2023 umefanya uzinduzi wa jukwaa la wadau wa ustawi wa mtoto mkoa wa njombe.
Mradi wa kizazi hodari kanda ya kusini ni mradi unaolenga kuimarisha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima, wenye mazingira hatarishi pamoja na vijana wa rika balehe wanaoishi katika jamii zilizoathirika zaidi na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Akielezea mafanikio ya mradi huo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Octoba 2022 hadi Septemba 2023 Mkurugenzi wa mradi huo Ndg Dorothy Matoyo amesema , mradi umefanikiwa kufikia wanufaika 25,097 katika mkoa wa Njombe na kati ya wanuafika hao watoto ni 316,702 na walezi ni 8,395. Kati yao 2,721 ni watoto na vijana wa rika balehe wanaoishi na virusi vya UKIMWI (VVU), ambao ni sawwa na asilimia 16% ya wanufaika wote.
Uzinduzi wa jukwaa hilo unalenga kuwashirikisha wadau mbalimbali baadhi ya changamoto ambazo mradi huu umekutana nazo ili kupata msaada wa wadau kufikia watoto wote katika huduma mbalimbali ikiwemo uhakika wa matibabu pale wanapougua pamoja ,elimu na kuwawezesha ili waweze kujikwamua badala yakutegemea msaada pekee.
“Ili kuhakikisha uendelevu wa huduma, tunahitaji kuwa na fungu maalumu kwa ajili ya kuwawezesha walezi na vijana wenye mawazo mazuri ya biashara ili waweze kujikwamua na kuwa msaada endelevu kwa kaya zao”
Baadhi ya changamoto zilizobainishwa na mradi wa kizazi hodari ni pamoja na watoto wengi kuishi kwenye nyumba zenye mazingira duni sana, Vijana wa umri wa miaka 15-18 kutokuwa shuleni, wananfunzi waliopo shuleni kukosa mahitaji muhimu kama sare, mabegi, viatu, na vifaa vya shule pamoja na mabinti wa rika balehe walio mashuleni kuhitaji msaada kuendelea kubaki shuleni kwa kupatiwa hifadhi salama wakati wa hedhi.
Aidha mkurugenzi wa mradi huo amesema wanahitaji msaada zaidi kwenye upande wa afya na kwamba kwa kuanza mradi umeweza kulipa kiasi cha shilingi 38,370,000/= kwa ajili ya kuwezesha bima ya Afya ya Jamii kwa Kaya 1,279 zenye jumla watoto 2,128 kwa kipindi cha kuanzia Septamba 2023 hadi Septamba 2024
“Pamoja na kuwa mradi umegharamia bima ya afya, hii ni sawa na asilimia 13% tu watoto walio kwenye mradi. Tunahitaji msaada wa wadau kufikia watoto wote ili waweze kupata uhakika wa matibabu pale wanapougua.”
Mradi wa kizazi kipya unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), kupitia mfuko maalum wa dharura wa kupambana na UKIMWI wa Raisi wa Marekani (PEPFAR), na unatekelwa na Deloitte kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Mandeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake Na Makundi Maalum ili kuhakisha mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi yanafanikiwa.
Mradi wa kizazi hodari Mkoani Njombe unatekelezwa katika Halmashauri zote sita ambazo ni Halmashauri ya wilaya ya Njombe Halmashauri ya Mji Njombe,Halmashauri ya Mji Makambako,Halmashauri ya wilaya ya Makete,Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe na Halmashauri ya wilya ya Ludewa.
Wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali walishiriki uzinduzi huo wa jukwaa la ustawi wa mtoto kwa mkoa wa Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe