Septemba 26, 2025 Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Njombe Mjini Bw.Samson Medda aliyepo katikati, ameshiriki kutoa elimu ya mpiga kura katika mjadala uliongazia ushiriki Jumuishi kwa kundi la Wanawake ,vijana na walemavu kwenye mchakato wa Uchaguzi.
Mjadala huo uliofanyika katika kituo cha redio Uplands Mjini Njombe,ulilenga kuangalia ushiriki wa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu katika mchakato wa uchaguzi, ambapo ulihusisha wawakilishi kutoka mashirika ya kiraia yaliyopewa jukumu na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kutoa elimu ya mpiga kura.
Washiriki walijadili changamoto ambazo zilikuwa zinayakabili makundi hayo na namna zilivyofanyiwa kazi kueleaka uchaguzi mkuu utakao fanyika Oktoba 29,2025 pamoja na mapendekezo kwa mambo ambayo bado hayajafanyiwa kazi ili kuhakikisha ushiriki kwa makundi yote unaboreshwa, na uchaguzi unakuwa wa haki na jumuishi kwa wote.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe