Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe Erasto Mpete Agosti 16,2023 amezungumza na wadau pamoja na watumiaji wa stendi kuu ya Mabasi Njombe nakutoa msisitizo wa utunzaji wa miundombinu ambayo ipo katika maeneo hayo.
Pamoja na kujadili chamgamoto mbalimbali za stendi kuu ya mabasi Njombe Mhe. Mpete .ametilia msisitizo suala la utunzaji wa mazingira na ili kuitunza na kuifanya idumu muda mrefu miundombinu ya stendi hiyo ambayo imetumia fedha nyingi za serikali.
"Niombe kila mtu awe mlinzi wa mwenzake watu wanapenda mahali ambapo ni pasafii na eneo likiwa chafu watu hawawezi kuja hivyo kukiwa na mazingira mazuri hata biashara zitauzika kutokana na usafi uliopo"Alisema Mhe Erasto Mpete M/Halmashauri ya Mji Njombe.
Kuhusu suala la mapato Mhe.Mpete amewaomba wafanyabiashara ambao wapo katika stendi hiyo kuhakikisha wanalipa mapato kwa wakati akiwahamasisha kujisajili kwenye mfumo mpya wa tausi ambao umekuja kurahisisha ukusanyaji wa mapato na kupunguza mianya ya rushwa .
Akiendelea kuzungumza na wadau hao pamoja na maafisa usafirishaji amewaomba watumiaji wastendi kuu kuhakikisha wanaimarisha ulinzi shirikishi kwa kuwa na mahusiano mazuri baina ya askari wa maeneo hayo na watumiaji wengine.
Kwa upande wake meneja wa Stendi Kuu Njombe Ndugu Kenan Maliga ameahidi kuendlea kutoa ushirikiano kwa wadau na watumiaji wa stendi hiyo katika changamoto ambazo zinawakabili wafanyabiashara waliopo eneo la stendi na kutengeneza mazingira rafiki kwa kila mtu .
Akihitimisha ziara yake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe amekabidhi vifaa vya michezo zikiwemo jezi kumi na nane (18) na mipira kumi (10) kwa timu ya Njombe Stand Fc iliyofuzu kucheza ligi ya mkoa wa Njombe.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe