Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Anthony Mtaka Januari 16,2024 wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lunyanywi na Mpechi, amewataka wanafunzi wote wa shule za Sekondari Mkoani Njombe ambao wanashiriki kuandaa vyakula nyumbani kuwa mabalozi wazuri wa kuhimiza lishe bora ndani ya familia.
"Mkawe mabalozi wazuri, naamini wengi wenu mnaandaa chakula, hakikisha mnakuwa na mchanganyiko wa mboga na matunda, na wakati mwingine jiulizeni je huu mlo ni bora? Muwe na bustani nyumbani, otesha mboga na matunda, na mnapowaandalia wadogo zenu uji Hakikisheni siyo uji mtupu, uwe na maziwa, karanga na virutubisho vingine" Alisema Mhe Mtaka.
Akiendelea kuzungumza Mhe. Mtaka amesema kuwa juhudi za Serikali ni kuhakikisha kila mwanafunzi anakuwa bora katika elimu akiwahimiza Wazazi, walezi, walimu wa shule zote za Mkoa wa Njombe kupanda matunda,mboga mboga Vinavyostawi katika maeneo ambayo wanaishi ili kuboresha lishe kwenye familia.
Haya yanajiri wakati Mkoa wa Njombe ukiwa kwenye kampeni maalum ya kupambana kutokomeza udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Kampeni hiyo imebeba kauli mbiu inayosema "Kujaza tumbo sio Lishe, Jali Unachomlisha"
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe