• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Njombe Town Council
Njombe Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

Mbunge Njombe Kusini atoa milioni 40 za mfuko wa Jimbo kuchochea miradi ya maendeleo Jimboni kwake

Tarehe iliyowekwa: December 12th, 2018

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Mfuko wa Jimbo iliyofanywa kwa lengo la kukagua na kupitisha miradi itakayosaidiwa na Mfuko huo, Mbunge wa Jimbo la Njombe Kusini Edward Mwalongo amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 40 kitatumika kununulia vifaa vya ujenzi kulingana na mahitaji ya mradi husika na vitagawiwa kwenye Kata 13 za jimbo hilo ili kuweza kuchochea na kuchangia kasi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mwalongo amesema kuwa vipaumbele vya Mfuko wa Jimbo ni kusaidia miradi ya afya, elimu pamoja na utawala hii ikihusisha ujenzi wa ofisi za kata na mitaa  mara baada ya kufanyika upembuzi yakinifu na kubaini mahitaji ya vifaa kwenye miradi iliyoibuliwa na wananchi na ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019 mfuko wa jimbo umefanikiwa kufanya jambo la upekee katika sekta ya elimu tofauti na vipindi vingine jambo ambalo limepokelewa kwa furaha na wanafunzi na uongozi wa Ruhuji shule ya Msingi.

“Kitu cha pekee ambacho Mfuko wa Jimbo umefanya katika mwaka huu wa fedha 2018/2019 ni kusaidia ujenzi wa jiko maalumu katika Shule ya Msingi Ruhuji ambalo litakua linatumia kuni kidogo, na rafiki wa Mazingira lakini pia ununuzi wa sufuria aina ya “Stainless steel”ambayo ni imara na haipati kutu na itatumika kwa muda mrefu. Hii itaonesha njia kwa Shule nyingine za Msingi na Sekondari katika Jimbo la Njombe kwamba jiko bora na sufuria bora liko Ruhuji Shule ya Msingi na wanaweza kufika pale kujifunza.”Alisema Mbunge wa Jimbo la Njombe Kusini Mhe. Mwalongo.

Sambamba na hilo Mwalongo amewaomba  Waheshimiwa Madiwani kutambua kwamba Mfuko wa Jimbo upo kwa ajili ya kuchochea maendeleo na kigezo kimoja wapo ni kwamba lazima wao wenyewe kwenye maeneo yao wawe wameanza.

“Mfuko wa Jimbo hauji kuwasha maendeleo unakuja kuchochea, vipo vijiji kama vitano kwenye Jimbo letu ambavyo havijawahi kupata ruzuku ya Mfuko wa Jimbo kwa kipindi chote hii ni kwa sababu maeneo yale hayana mradi wa aina yoyote. Niwaombe vijiji hivyo wananchi kwa kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani kuibua miradi na waanze utekelezaji na itakapofikia kipindi cha ufadhili wa mfuko wa Jimbo tutaikagua na ikikidhi vigezo tutawapatia vifaa vya ujenzi ili miradi hiyo ikamilike na ianze kutumika kwa manufaa ya wananchi kwa ujumla” Mwalongo alisema

Kwa upande wake Daniela Msemwa ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Makowo Kata ya Makowo amesema kuwa wanashukuru uwepo wa Mfuko wa Jimbo na anampongeza Mhe. Mbunge wa Jimbo la Njombe Kusini kwa jinsi anavyosimamia mfuko huo kwani Mfuko huo umekuwa ukichochea maendeleo katika Kata yao na umewahamasisha wananchi wengi kujitolea kuchangia shughuli za maendeleo kwenye Kata hiyo.

Kamati hiyo pia imeshauri ni vyema Wataalamu wa Halmashauri kuwa na mawasiliano ya karibu na Wananchi ili kuweza kutoa ushauri wa kitaalamu ikiwemo matumizi sahihi ya viwango vya ujenzi na michoro ili kuepuka lawama na uharibifu wa rasilimali za wananchi.

Mfuko wa Jimbo ulifanikiwa kutembelea miradi 40 katika Kata 13 zilizopo kwenye Halmashauri ya Mji Njombe na imefanikiwa kuipitisha miradi 21 katika kata hizo ambazo zitapatiwa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Tsh. Milioni 38 na Milioni mbili zitatumika kwa ajili ya kuchangia mradi wa ujenzi wa vyoo vya kisasa vya wasichana katika shule ya Msingi Mpechi mradi ambao unatekelezwa na Umoja wa Wabunge Wanawake katika kila Jimbo Nchi nzima.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI,UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI. April 25, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA MPIGA KURA. December 20, 2024
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA NJOMBE MHE. JUMA SWEDA ATOA WITO KUHUSU CHANJO YA PILI YA POLIO.

    April 29, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA NJOMBE MJINI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA

    April 24, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA NJOMBE KUKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 04, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe awaonya wenyeviti kuhusu uharibifu wa miradi ya maendeleo

    February 15, 2025
  • Angalia zote

Video

WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KUJITUMA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe