Juni 17,2024 Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mhe.Victoria Mwanziva amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa Katika Kata ya Matola ,Kijiji cha Boimanda.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Mji utapitia, kukagua na kuzindua miradi 6 na shughuli 2 kati ya hizo 1 ikiwa ni ukaguzi wa klabu ya kupambana na Rushwa na Shughuli nyingine ni uzinduzi wa wimbo wa uhamasishaji wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kwa upande wa miradi Mwenge wa Uhuru utazindua miradi 3 na kukagua miradi 3.
Katika kata ya Matola Mwenge wa Uhuru utazindua vyumba 3 na ofisi 1 vyenye thamani ya shilingi 79,050,552.00 katika Shule ya Msingi Boimanda.
Hata hivyo katika kata ya Uwemba Mwenge wa Uhuru utafanya Ukaguzi wa Msitu wa asili wa Isililo wenye ukubwa wa hekta 58.8 wenye thamani ya shilingi 189,229,000
00 pamoja na kugawa mizinga 10 kwa kikundi cha wafugaji wa nyuki.
Aidha katika kata ya Yakobi Mwenge wa Uhuru utakagua shamba la parachichi la mwekezaji Frank Msuya lenye ukubwa wa ekari 200 ambalo uwekezaji wake ni shilingi billioni 1.
Katika kata ya Mjimwema Mwenge wa Uhuru utafanya uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Amoil ambacho uwekezaji wake ni zaidi ya millioni 721,083,707.00
Wakati huo huo katika, kata ya Njombe Mjini Mwenge wa Uhuru utafanya Ukaguzi wa kikundi cha vijana cha Sungura Njombe (SUNJO) ambao ni wanufaika wa mikopo inayotolewa na Halmashauri ambacho mpaka sasa kikundi kina thamani ya shilingi milioni 30.
Na katika kata ya Ramadhani Mwenge wa Uhuru Utazindua jengo la mama na mtoto katika hospitali ya Mji Njombe (Kibena) ambalo limejengwa kwa shilingi milioni 173 ,167,000.00
Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 inasema "Tunza mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe