Shamba la parachichi la Mwekezaji Frank Msuya lenye ukubwa wa hekari 200 na thamani ya uwekezaji wake ikiwa ni Bilioni 1 lililopo kata ya Yakobi kijiji cha Nundu ,limekaguliwa na kuwekewa kibao cha ukaguzi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Juni 17,2024.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Godfrey Mnzava ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwajali wawekezaji nakuwafikishia mahitaji muhimu kwenye maeneo yao ya uwekezaji ikiwemo,Miundombinu ya barabara ,maji na umeme pamoja na ruzuku kwenye mbolea na viatilifu vinavyotumika kwenye kilimo.
Uwekezaji katika shamba hilo la linalofahamika Havila Farm ulianza mwaka 2010 kwa kupanda miche 1,235 kwenye ekari 16. Hadi kufikia mwaka 2023, ekari 115 zimepandwa miche ipatayo 12, 000
Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2024 zinaongozwa na kaulimbiu isemayo "Tunza mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu.
MWENGE WA UHURU WARIDHISHWA NA UWEKEZAJI KATIKA KILIMO CHA ZAO LA PARACHICHI.
Shamba la parachichi la Mwekezaji Frank Msuya lenye ukubwa wa hekari 200 na thamani ya uwekezaji wake ikiwa ni Bilioni 1 lililopo kata ya Yakobi kijiji cha Nundu ,limekaguliwa na kuwekewa kibao cha ukaguzi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Juni 17,2024.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Godfrey Mnzava ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwajali wawekezaji nakuwafikishia mahitaji muhimu kwenye maeneo yao ya uwekezaji ikiwemo,Miundombinu ya barabara ,maji na umeme pamoja na ruzuku kwenye mbolea na viatilifu vinavyotumika kwenye kilimo.
Uwekezaji katika shamba hilo la linalofahamika Havila Farm ulianza mwaka 2010 kwa kupanda miche 1,235 kwenye ekari 16. Hadi kufikia mwaka 2023, ekari 115 zimepandwa miche ipatayo 12, 000
Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2024 zinaongozwa na kaulimbiu isemayo "Tunza mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".
@njombe_rs @kissagwakisakasongwa @ms_mhaiki
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe