Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg.Godfrey Mnzava baada ya ukaguzi wa nyaraka na Miundombinu amezindua mradi wa vyumba vitatu (3) vya Madarasa na Ofisi moja (1) katika Shule ya Msingi Boimanda wenye gharama ya shilingi Milioni 79,050 552.00 ikiwa ni fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri, wadau na nguvu za wananchi.
Mradi huu umejengwa kwa kutumia utaratibu wa Force Account na Kiasi cha Tsh 79,050,552.00 kilitumika kukamilisha mradi huu ambapo Tsh 54,426,368.00 ni Mapato ya Ndani ya Halmashauri, Tsh 1,275,000.00 ni Mfuko wa Jimbo, Tsh 4,190,000.00 ni Mdau wa Maendeleo, Tsh 818,132.00 Serikali kuu na Tsh 18,341,052.00 ni nguvu za wananchi.
Kukamilika kwa mradi huu kumewezesha wanafunzi (350) na walimu (7) kupata mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia nakuondoa changamoto ya mrundikano wa wanafunzi darasani.
Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2024 zinaongozwa na kauli mbiu isemayo "Tunza mazingira na shiriki Uchaguzi kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu ".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe