Akizungumza katika Uwanja wa Mkwakwani, Jijini Tanga, Mhe. Katimba amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini kuhakikisha wanatenga fedha za kutosha katika vitengo vya utamaduni na michezo na kuhakikisha mgawanyo wa fedha za ruzuku kila mwezi utolewa kwa kitengo hicho kama ilivyo kwa idara nyingine,jambo ambalo litawawezesha watumishi kushiriki ipasavyo katika mashindano hayo ikiwa ni sehemu ya kujenga mshikamano na afya bora kwa watumishi.
Amebainisha kuwa mwaka huu Halmashauri 15 zimeshiriki akiwataka Wakurugenzi ambao hawajawaleta watumishi wao kuhakikisha wanawasilisha wachezaji kabla ya mashindano kuhitimishwa.Amesisitiza watumishi kuendelea kufanya mazoezi kwa afya na kuanzia mwakani Halmashauri zote zinatakiwa kushiriki bila kukosa.
“Watumishi wa serikali waendelee kufanya mazoezi kila siku ili kujenga afya na kuimarisha utendaji kazi"Alisema Mhe.Katimba.
Ametoa wito kwa washiriki kuhakikisha wanatoa elimu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi mbalimbali litakalofanyika Oktoba 29, 2025.
“Kama ilivyo kaulimbiu ya mashindano haya,huu ni mwaka wa uchaguzi, michezo hii ni jukwaa la kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura onesheni uzalendo kwa kuchagua viongozi bora watakaoiwezesha serikali kusonga mbele katika maendeleo ya michezo mbalimbali, sambamba na kulinda maslahi ya Taifa,” alisema Mhe. Katimba.
Pia amekumbusha kuwa mashindano haya ni kwa ajili ya watumishi pekee, akipiga marufuku kwa watu wasiokuwa watumishi (‘mamluki’) kushiriki. “Iwapo itabainika kuna Halmashauri imeruhusu wachezaji wasio watumishi, hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa kanuni za shirikisho,” alisisitiza.
Mashindano ya mwaka huu yanaenda na kaulimbiu ya "Jitokeze kupiga kura kwa maendeleo ya Michezo " yamehusisha michezo mbalimbali 15 na maonesho ya sanaa yakilenga kukuza vipaji, mshikamano na afya kwa watumishi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe