Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuboresha huduma ya usafiri wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga(m-mama), ambapo kuanzia Julai 2024 namba ya dharura ya bure 115 itaanza kutumika rasmi ngazi ya jamii badala ya kutumika kwenye vituo vya kutolea hiduma za afya pekee.
Hayo yamebainishwa Julai 10,2024 wakati wa mafunzo kwa watoa elimu ya afya kwa umma na Maafisa mawasiliano Mkoani Njombe, kuhusu mfumo wa M-mama na kuanza kutumika kwa namba ya dharura ya bure 115 ngazi ya jamii.
Wajibu mkuu kwa walengwa wa mafunzo hayo ni kuhakisha jamii inakuwa na uelewa kuhusu huduma ya usafiri wa dharura ya m-mama na matumizi ya sahihi ya namba 115 ili kumsaidia mlengwa ambaye ni mjamzito na mtoto mchanga mwenye umri 0 -siku 28 kwa wakati.
Mfumo wa m-mama, ni mfumo maalumu ulioanzishwa kwa ajili yakutoa huduma ya usafiri wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga ili kupunguza vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga.
Pamoja na mafunzo hayo walengwa kwa kushirikiana na timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya,TAMISEMI na shirika la Pathfinder waliweza kuandaa mpango kazi wa Mkoa wa kuelimisha umma kuhusu m-mama na namna inavyofanya kazi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe