Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mheshimiwa Anthony Mtaka Mei 14,2024 amekemea vikali kufanyika kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo kulisha mifugo pamoja na kufanya kilimo kwenye vyanzo maji.
Hayo yamejiri kwenye ziara aliyoifanya Wilaya ya Ludewa kata ya mavanga, kijiji cha mavanga ambapo wananchi wililamikia uchafu wa maji kwenye mradi unaotekelezwa kijijini hapo wenye thamani ya zaidi ya bilioni 1.3 utakaohudumia wakazi wapatao 5,000.
"Ni kweli dinga zipo,lakini maji yanachafuliwa na shughuli za kibinadamu ,mtashikana uchawi bure lakini wachawi ni sisi wenyewe ,Mhe. Rais ameshatimiza wajibu wake fedha zimefika,wekundu wa maji unasababishwa na ngo'mbe" Alisema Mhe. Mtaka.
Mhe. Mtaka ametoa wito kwa Viongozi wa kijiji na kata kushirikiana katika kujiwekea sheria ndogondogo kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji kwa faida ya kijiji na taifa kwa ujumla.
“Kwenye WADC wekeni sheria ,mkitaka mtusaidie watu wenye ngo'mbe kwenye eneo la chanzo watoe ngo'mbe ,watu wanaolima kule karibu na chanzo watoke,kwa sababu kuna siku mradi utakamilika maji yatakuwa hayatoki chanzo kitakuwa kimekauka.”Alisisitiza
Aidha amempongeza mkandarasi mzawa anaetekeleza mradi huo Emirate Builders Co. Ltd kwa kuonesha uzalendo.
“Tunahitaji wakandarasi kama Emirate ametekeleza mradi mpaka hatua hii kwa malipo ya asilimia 15,tungekuja hapa tukute mawe mashimo na picha nzuri ya tenki la maji lakini ametumia fedha ya mtaji wake ,lakini pia amekubali maboresho ya nyongeza,mnapopata miradi mingine watu wa hivi wapeni .”
Utekelezaji wa mradi huo wa kijiji cha Mavanga unalenga kuimarisha miundombinu ya mradi wa awali kwa kujenga miundombinu mipya, kupanua mtandao wa maji na kuongeza huduma ya maji kutoka kwenye chanzo kipya cha mto Msolwa.
Naye mhandisi wa mradi huo Ombeni Mwanri kutoka kampuni ya Emirate Builders Co Ltd alisema mradi huo umefikia asilimia 97 na kuahidi kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa ili mradi ufanye kazi kwa ufanisi unaotakiwa.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe