Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Mhe .Chifu Deo Mwanyika ametoa bure mitambo ya kuchimba barabara zote ambazo zina changamoto ndani ya Halmashauri ya Mji njombe.
Mhe. Mwanyika amesema hayo Januari 9 ,2023 wakati akizungunza na wananchi wa Mtaa wa Nazareth na Melinze katika mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Aidha Mhe.Mwanyika amesema kuwa amekuwa akipigania kwa udi na uvumba kuhakikisha fedha za maendeleo zinafika kwa wakati katika Halmashauri ambapo mpaka sasa vituo vya afya ,barabara pamoja na ujenzi wa miradi mikubwa ya maji inaendelea Lugenge ,Ngalanga na maeneo mengine.
"Ndugu zangu kazi ya ubunge ni kupigania rasilimali; rasimali fedha na rasimali watu ambayo inatolewa ngazi kubwa ya kitaifa lakini vilevile kazi ya Mbunge ni kuhakikisha changamoto zenu zinapatiwa ufumbuzi kwani nina nafasi ya kuwasiliana na Mawaziri" Ameongeza Mwanyika.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe Erasto Mpete amesema wataaendela kutatua kero na kufikisha huduma ambazo wananchi wanahitaji huku akiweka bayana namna ilani ya mwaka 2020-2025 ilivyotekelezwa kwa kasi kubwa.
Naye Diwani wa Kata ya Mji Mwema Mhe Nestory Mahenge amewaomba wazazi na walezi kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao ambayo imekuwa ikichangia kuharibu maadili ya watoto na kupelekea kutofanya vizuri katika masomo yao.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe