Halmashauri ya Mji Njombe imeshika nafasi ya kwanza kwenye tuzo za usafi wa mazingira mwaka 2023 kipengele cha Miji nakupewa kombe na fedha shilingi milioni 5.
Aidha Hospitali ya Mji wa Njombe Kibena imeshika nafasi ya pili kwenye tuzo za usafi wa mazingira kwenye kipengele cha hospitali za Wilaya nakupatiwa cheti na fedha shilingi milioni 2.
Zawadi hizo zimekabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Mpango ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo lililofanyika viwanja vya stendi ya zamani Halmashauri ya Mji wa Kibaha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Timu ya Halmashauri ya Mji Njombe iliyohudhuria sherehe ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa mashindano ya afya na usafi wa mazingira imeongozwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe Erasto Mpete pamoja Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Njombe Daktari Jabil Juma.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe