Halmashauri ya Mji Njombe imekuwa Halmashauri ya pili kitaifa nakupatiwa tuzo katika kundi la Miji kwenye Usimamizi bora wa Rasilimali watu.
Tuzo hiyo imetolewa Oktoba 11,2023 katika Mkutano wa wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu katika Utumishi wa Umma unaofanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 11 hadi 13, 2023 katika kituo cha kimataifa cha mikutano Arusha (AICC)
Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ndugu George Simbachawene kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Ndugu Samson Medda.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe