Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe Ndugu Kuruthumu Sadick amesema Halmashauri ya Mji Njombe inaunga mkono programu ya kuwawezesha vijana kwenye fursa za kilimo inayoratibiwa na kusimamiwa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Njombe.
Akizungumza katika kongamano la fursa za vijana Wilaya ya Njombe lililo andaliwa na Mkuu Wilaya ya Njombe Mhe.Kissa Gwakisa Kasongwa, Ndugu Kuruthum Sadick amewakaribisha wanaotaka kuwekeza ndani ya Halmashauri ya Mji Njombe na kutoa wito kwa vijana kuwa mstari wa mbele kuchangamkia fursa za kiujasiriamali ambazo zinajitokeza katika maeneo ambayo wanaishii
Aidha amesema Halmashauri ya mji Njombe imetenga hekta 40 kwa ajili ya vijana kuwekeza katika shughuli mbalimbali za maendeleo haswa kilimo ili kuweza kujikwamua kiuchumi .
Kwa upande wake Enembora Lema Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Mji Njombe amewashauri vijana wote hukakikisha wanajiunga na vikundi vya kiujasiriamali kutokana na Halmashauri kutenga mikopo wezeshi kwa ajili Vijana ,Wanawake na Walemavu.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe