Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka leo amepokea ugeni kutoka katika Jiji la Miltenberg Nchini Ujerumani ikiwa ni hatua za awali za uanzishaji wa mradi wa kuhakikisha kuwa Njombe inakua safi na kijani, lengo kuu la pili ikiwa ni kuweka nishati mbadala rafiki wa mazingira katika maeneo ya umma kwa kuongeza matumizi ya nishati jua (solar) kwenye maeneo hayo. Ushirikiano ambao ulioanzishwa kati ya Mji wa Miltenberg na Halmashauri ya Mji Njombe.
Akizungumza mara baada ya kupokea ugeni huo uliofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha na kuelezea adhma ya mashirikiano hayo, Mtaka alisema kuwa Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa Mikoa Tanzania ambayo inafursa nyingi za kiuchumi ikiwemo kilimo cha matunda na hivyo ujio huu umekuja katika wakati muafaka ambapo moja ya vipaumbele vya Mkoa ni kuhakikisha kunakuwa na mazingira bora na wezeshi kwa sekta binafsi kufanya shughuli za kiuchumi Mkoani Njombe.“Sisi kama Mkoa pia tunalojukumu kubwa la kuhakikisha tunaboresha Sekta ya Elimu kwa Wanafunzi wetu kwa kuwa na ufaulu bora hivyo ni vyema tukaona namna bora ya kuwa na programu za kubadilisha uzoefu katika elimu kati ya Mji wa Miltenberg ili kuweza kufanya maboresho lakini pia kujifunza vitu vipya kupitia program hizo hali kadhalika kwa Wafanyabishara ambao wataweza kuja kwetu na sisi kwenda kwao kujifunza ili kuimarisha biashara zao.”Alisema Mtaka
Aidha, kupitia mradi huo manufaa mengine yatakayotokana na ushirikiano huo ni pamoja na kuhakikisha kuwa uboreshaji wa ukusanyaji na uhifadhi wa taka ngumu unafanyika kwa njia za kisasa ambazo hazitaleta athari kwa mazingira na kusarifu taka ngumu na kuzifanya kuwa mbolea na nishati ya umeme katika Mji wa NjombeMara baada ya kukamilika kwa ziara yao ya siku tano Mjini Njombe ugeni huo utawasilisha andiko maalum
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe