Maafisa lishe wa Halmashauri ya Mji Njombe na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe wametakiwa kuendelea kushirikiana kwa karibu na watendaji wa kata kuongeza hamasa ili kupata idadi kubwa ya wazazi na walezi wanaojitokeza kushiriki kwenye siku za Afya na Lishe kwenye vijiji na mitaa(SALIKI).
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe Kissa Gwakisa Kasongwa Agosti 12,2024 kwenye kikao cha tathmini ya utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa Lishe kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024
"Tuongeze msukumo kwenye SALIKI uwe mkubwa ,tujitahidi hamasa iwe kubwa ili wananchi waweze kushiriki kwa wingi ili elimu iwafikie."Alisema Mhe.Kissa Gwakisa Kasongwa, Mkuu wa Wilaya ya Njombe.
Kutokana na changamoto ya hali duni ya Lishe inayopelekea udumavu kwa watoto ,Mkoa wa Njombe unaendelea na Kampeni ya kupambana udumavu ya Lishe ya Mwanao ,Mafanikio yake ,yenye kaulimbiu isemayo "Kujaza tumbo siyo Lishe jali unachomlisha", iliyozinduliwa Disemba 22,2023 na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe .Anthony Mtaka ambapo Halmashauri ya Mji Njombe imepiga hatua na hali ya udumavu imepungua kutoka asilimia 45 mwaka 2022 hadi asilimia 42.4 mwaka 2024 hii ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo UNICEF na TFNC.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe