Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Mji Njombe, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Erasto Mpete, imetoa pongeza kwa Mkurugenzi na menejimenti ya halmashauri, kwa kazi bora ya kuandaa taarifa za mwisho za hesabu kwa mwaka wa fedha ulioishia Tarehe 30 Juni 2023.
Maandalizi hayo yameiwezesha Halmashauri ya Mji Njombe kuibuka mshindi wa nafasi ya tatu kitaifa kati ya halmashauri 187, na hivyo kutunukiwa tuzo ya Ngao ya Hesabu Bora katika hafla iliyoandaliwa na Bodi ya Wahasibu na wakaguzi Tanzania.
Mhe. Mpete alisisitiza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya ushirikiano mzuri, uwajibikaji, na juhudi za pamoja katika kuhakikisha uwazi na weledi katika usimamizi wa fedha za umma.
Alitoa wito kwa menejimenti kuendelea kudumisha utendaji bora ili kuimarisha maendeleo ya halmashauri na ustawi wa wananchi.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe