Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof.Adolf Mkenda Septemba 20,2024 ,akiwa katika ziara ya kukagua miradi Mkoa wa Njombe,ameweka jiwe la msingi kwenye shule mpya ya sekondari Makowo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 583, inayohudumia watoto wa kijiji cha Makowo ,Ngelamo na Mamongolo katika Halmashauri ya Mji Njombe mkoani Njombe.
Awali kata ya Makowo haikuwahi kuwa na shule ya Sekondari hivyo kupitia mradi wa Sequip Shule mpya ya Sekondari Makowo imejengwa ili kuboresha mazingira ya elimu na kupunguza msongamano na changamoto kwa watoto wa vijiji vya Makowo ya kutembea umbali mrefu zaidi ya kilomita 5 kwenda shule iliyopo kata ya jirani, jambo ambalo lilisababisha wengi wao kutokupenda shule na wengine kuacha masomo.
Shule mpya ya Sekondari Makowo iliyopo kilomita 85 kutoka makao makuu ya Halmashauri tayari imeanza kutumika ikiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza 92 wavulana wakiwa ni 38 na wasichana 54.
Miundombinu iliyojengwa shuleni hapo inajumuisha Jengo la utawala moja (1),vyumba vya madarasa ya kisasa nane (8), ofisi mbili (2), maabara tatu (3) za sayansi, maktaba,chumba cha kompyuta (ICT Room) na miundombinu mingine muhimu ikiwemo matundu ya vyoo na kichomea taka.
Aidha ili kuendelea kuboresha mazingira kwa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo wanachi wa Kata ya Makowo tayari wametoa fedha shilingi milioni 27 kwa ajili ya ujenzi wa bweni huku Halmashauri ya Mji Njombe kupitia fedha za mapato ya ndani ikiwa tayari imetoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya bweni ambalo linatarajiwa kukamilika nakuanza kutumia ifikapo Januari 2025.
@wizara_elimutanzania @professoradolfmkenda @ortamisemi @kissagwakisakasongwa @ccm_dijitali @njombe_rs @uvccm_wilaya_njombe @uvccm_njombe @dc_njombe @ikulu_mawasiliano @maelezonews @samia_suluhu_hassan
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe