Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Judica Omary amesema kuwa bado elimu zaidi inatakiwa kwa Wananchi juu ya namna bora ya uhifadhi wa taka kwa kuzitenganisha na kuachana na tabia ya kuhifadhi taka zote sehemu moja.
Akizungumza wakati alipokutana na ugeni kutoka Miltenberg Ujerumani ambao ni Mji rafiki na Halmashauri ya Mji Njombe, Judica amesema kuwa ni vyema elimu ikaendelea kutolewa na Wananchi kujengewa uwezo juu ya umuhimu wa utunzaji wa taka kwa kuzitengeanisha kwa kuanzia katika hatua za awali kwa Wanafunzi mashuleni ili kuweza kutumia maarifa hayo majumbani kwao kwani mabadiliko hayaanzi kwa mara moja bali huanza kidogo kidogo.
“Katika muda wa siku tano ambao mtakuwa hapa Mjini Njombe natumaini mtaona hali halisi tuliyo nayo, lakini kuweza kutoa maoni na ushauri wa namna bora ya kuweza kuboresha ukusanyaji na uhifadhi wa taka ngumu katika Mji wa Njombe. Ili kupitia mradi ambao utakaoanzishwa kuona ni kwa namna gani yale ambayo hayatafanikiwa kutekelezwa kutokana na ukubwa wake yaweze kuwa ni sehemu ya mradi utakaoweza kuanzishwa ili Mji wa Njombe uweze kuwa mfano bora kwenye uhifadhi na utunzaji wa mazingira.”Alisema Judica
Katika hatua nyingine Judica amesema kuwa changamoto nyingine ni kuwa katika kipindi cha kiangazi kumekuwa na moto ya mara kwa mara inayosababisha kuungua kwa misitu na hivyo kupelekea uchafuzi wa mazingira ambapo licha ya kuwa Mkoa,Wilaya na Halmashauri zimeweka sheria mbalimbali za usimamizi wa maandalizi ya mashamba ambapo bado Wanananchi wamekuwa na muitikio wa kulega lega kwenye utekelezaji wa sheria za uhifadhi na ulinzi wa mazingira
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe