Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Balozi Dkt .Pindi Chana ametoa rai kwa Wafanyabiashara wa Mkoa Njombe kuhakikisha wanatumia fursa mbalimbali za uchumi katika Tamasha la pili la Utamaduni ma Michezo kitaifa ili kujiingizia kipato.
Amesemahayo Mhe Balozi Pindi Chana alipokuwa akizungumuza na wananchi wa Mkoa wa Njombe katika Uzinduzi wa Tamasha la Pili la Kitaifa la Utamaduni Mkoa wa Njombe ambapo amewaomba wakazi wa mkoa wanjombe kuhakikisja wanatumia fursa hiyo ili kujikuhakikisha wanapata faida katika biashara zao ambazo wanaziunza .
Akiendelea kuzungumza Mhe Balozi Pindi Chana amesema kuwa Wizara ya Utamaduni Sanaaa na michezo wamejipanga kuhakikisha wanatanua wingo kwa kila mkoa katika uchumi na kuwawezeaha vijana katika utamaduni ambapo kwa sasa asilimia 30%wamejiajili kupitia sekta ya Utamaduni ,Sanaa na michezo .
Katika uzinduzi huo Mhe Pindi Chana amewaomba Watanzania kuhakikisha wanadumisha utamaduni wa asili na kuilinda amani ya nchi yetu ambayo ni Tunu ya Taifa letu .
Kwaupande wake Mhe Kissa Gwakisa Kasongwa Mkuu wa wilaya Njombe ambaye alimwakilisha mkuu Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka katika uzinduzi huo ameishukuru serikali kwa kuleta tamasha hilo katika mkoa wa njombe huku akiwaomba wananchi wa mkoa huo kunufaika na tamashailo ambalo limefungu fursa mbalimbali za uchumi kwa wananjombe
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Antonia Sizya amesema kuwa Maadili yakizingatiwa yatasaidia Kuiweka Jamii ya Watanzania pamoja huku Machifu wenyeji wa Mkoa wa Njombe Wakisema Kuwa Ujio wa Tamsha Hilo umekuwa na Faida Kubwa.
Kauli Mbiu ya Tamasha la pili la utamaduni inasema, "Utamaduni ni Msingi wa Maadili, Tuulinde na Kuendeleza.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe