Rais Samia Suluhu Hassan ameulekeza uongozi wa Mkoa wa Njombe kuweka kituo maalumu cha kulelea watoto katika soko kuu la Njombe kwa ajili ya watoto ambao wazazi wao wanafanya biashara kwenye soko hilo.Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumatano Agosti 10, 2022 alipotembelea na kuzindua soko hilo la kisasa akiwa ziarani mkoani Njombe.
“Nimepita hapa nimeona wanawake wengi wana watoto wadogo mgongoni, wengine wanacheza chini mama zao wanaendelea na biashara.Ninachoona kuna haja ya kuwa na eneo maalum ambalo watoto hawa watalelewa ili kuwapa nafasi wazazi wao kuendelea na biashara,” amesema.
Hata hivyo, Rais Samia amewataka wanawake watakaokitumia kituo hicho kuwa tayari kuchangia huduma za kuwatunza watoto hao.“Tukubaliane lazima tuchangie kidogo, maana watakuwepo watoa huduma na pia watoto watahitaji mahitaji mbalimbali ni vyema tukawa tayari kuchangia,” amesema Rais Samia.
Rais anaendelea na Ziara yake Mkoani Njombe ambapo mara baada ya kuzindua soko kuu Njombe atatembelea kiwanda Cha MIWATI TANWAT na baadaye kushiriki katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya sabasaba na kuzungumza na Wananchi wa Njombe
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe