• Malalamiko |
    • Barua Pepe |
Halmashauri ya Mji Njombe
Halmashauri ya Mji Njombe

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Halmashauri ya Mji Njombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu na uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mazingira na Usafishaji
      • Ununuzi
      • TEHAMA na Takwimu.
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Election
      • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Utamaduni,Sanaa na Michezo
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Madini
    • Kilimo na Mifugo
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • Kilimo na Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Afya,Elimu na Maji
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Vikao vya Kisheria
      • Vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kumuona Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu za Maombi mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida

RAIS SAMIA AZINDUA BARABARA YA MAKETE NJOMBE

Tarehe iliyowekwa: August 9th, 2022

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete kutafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumanne Agosti 9, 2022 wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo akisema barabara hiyo ina umuhimu, kwani pia itaunganisha wilaya hiyo na mikoa na nchi zinazopakana na Tanzania.

Mbali na kufungua masoko, Rais Samia amesema pia barabara hiyo itafungua utalii hasa kutokana na hifadhi zilizopo wilayani humo.

"Lakini niwaambie jambo moja barabara hii ya Makete tumeisubiri kwa muda mrefu sana na fedha iliyotumika kujenga barabara hii ni zaidi ya Sh100 bilioni kwa kilomita zote 107.

“Ombi langu kwa Wanamakete ni kuilinda barabara hii," amesema Samia.

Amewaonya watu wenye tabia ya kuchimba mchanga na madini chini au kando ya barabara, kuacha mara moja tabia hiyo.

Advertisement

Awali akizungumza, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali inafahamu kuwa wananchi wa wilaya hiyo wanapata mahitaji yao kwa kiasi kikubwa kutoka Mkoa wa Mbeya, hivyo ilikuwa ni lazima barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 203.6 kujengwa.

Amesema mkandarasi wa kujenga barabara hiyo amepatikana na anatarajia kuanza kazi mwezi ujao kwa kujenga kipande cha kutoka Kitulo mpaka Inyuho chenye urefu wa kilomita 36.3.

"Mheshimiwa Rais tumechagua kipande hiki kwa sababu eneo hilo ni korofi sana na mvua ikinyesha halipitiki," amesema Mbarawa.

Amesema vipande vinavyofuata mkandarasi atawekwa kuanzia Makete ili wakutane na yule anayeanzia Kitulo ili barabara hiyo iwe kuwa na lami asilimia mia moja.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Rogatus Mativila amesema barabara hiyo inaunganisha makao makuu ya mkoa wa Njombe na wilaya ya Makete ni muhimu kwa wananahci wa mkoa huo.

Matangazo

  • KUITWA KAZINI NA MAFUNZO TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI. October 21, 2025
  • TANGAZO LA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI. October 19, 2025
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 May 19, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA. April 18, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MTAKA AONGOZA MAOMBI YA AMANI KWA TAIFA.

    November 07, 2025
  • MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO NJOMBE MJINI AFUNGUA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA .

    October 26, 2025
  • MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA 366 WAAPISHWA NA KUPATIWA MAFUNZO JIMBO LA NJOMBE MJINI.

    October 25, 2025
  • KUBWA KULIKO KUWAHI KUTOKEA NJOMBE MJINI

    October 20, 2025
  • Angalia zote

Video

TANGAZO LA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Huduma za Afya
  • Huduma za Elimu
  • Huduma za Biashara

Kurasa Mashuhuri

  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Mkoa wa Njombe
  • Watumishi portal
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 na vyuo

Watazamaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.

    Sanduku la Posta: S.L.P 577

    Simu ya Mezani: 026-2968833

    Simu ya Mkononi: 026-2968833

    Barua Pepe: td@njombetc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe