Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe.Erasto Mpete Agosti 30 ,2024 ameongoza kikao Maalum cha Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Njombe kwa ajili ya kujadili rasimu ya Hesabu za Mwisho wa mwaka wa fedha 2023/2024.
Katika kikao hicho, wajumbe wa Baraza la Madiwani wamepitia na kujadili kwa kina masuala yote ya kifedha kwa mwaka wa fedha uliomalizika kwa lengo la kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma.
Mwenyekiti alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi na watendaji wa Halmashauri ili kuhakikisha kuwa rasimu hiyo inakidhi vigezo vyote vya kisheria na kiutendaji.
Pia, alitoa wito kwa wajumbe kuhakikisha wanazingatia maoni na mapendekezo yaliyotolewa katika kikao hicho kwa ajili ya maboresho ya mwisho kabla ya kuwasilisha hesabu hizo kwa mamlaka husika.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe