Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema sensa ya watu na makazi imeanza vizuri na na kwamba ameridhishwa na usiri wa makarani katika uchukuaji wa taarifa. Hayo ameyasema leo Agosti 23 wakati alipozindua sensa katika hospital ya Halmashauri ya mji Njombe kisha kutembelea eneo la mizani lililopo mjini Makambako kukagua kazi hiyo inavyoendelea mkoani hapa.
Amesema sense inafanyika kwenye maeneo yote hata barabara makarani wapo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha watu wote wanahesabiwa. "Kwa maana taarifa za makarani wetu mambo yote yanakwenda vizuri na ushirikiano unatolewa kwa wananchi," amesema Mtaka.
Msimamizi wa sensa mkoa wa Njombe, Sarun Njipay amesema makarani wanaendelea kuhesabu watu kulingana na miongozo iliyotolewa ili wananchi watoe taarifa zilizo sahihi.
"Tumeanza kuhesabu makundi mbalimbali ili kuhakikisha hakuna mtu yoyote anaachwa bila kuhesabiwa," amesema Njipay.
Baadhi ya wananchi waliosabiwa wamesema utaratibu uliowekwa ni mzuri kwani utawawezesha makarani kuhesabu watu wote bila ya kuacha wengine.
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe