Tarehe 11 Oktoba 2024 ,Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Anthony Mtaka amejiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Mtaa wake wa Lunyanywi uliopo Kata ya Mji Mwema , Halmashuauri ya Mji Njombe.
Akizungumza mara baada yakujiandikisha na wananchi waliofika kwenye kituo hicho Mhe.Mtaka ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Njombe kujiandikisha ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Tarehe 27 Novemba 2024 .
" Niwaombe sana wananchi wote wa mkoa wa Njombe kila mtu mwenye sifa ahakikishe anajiandikisha kwenye orodha,sifa ni chache uwe mtanzania ,mwenye umri wa miaka 18 na zaidi ,mkazi wa eneo husika na mwenye akili timamu uchaguzi huu ni muhimu sana."Alisema Mhe.Anthony Mtaka -Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
Pia, amesisitiza kwamba kadi ya mpiga kura haitatumika katika uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, na amewataka wananchi kutumia vizuri muda wa siku 10 za kujiandikisha ili kuwawezesha kuwa na sifa ya kuchagua viongozi wanaoweza kufanya maamuzi sahihi.
Viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya siasa pia wamehimizwa kutumia nafasi zao kuhamasisha waumini wao kujiandikisha na kushiriki kwenye uchaguzi.
Aidha ametoa wito kwa wale wanaopanga kugombea kuchukua fomu katika maeneo yao, huku vyama vya siasa vikitakiwa kuwasimamisha wagombea bora.
Zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Limeanza Rasmi na litaemdelea mpaka Tarehe 20 Oktoba 2024.
"Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi Jitokeze Kushiriki Uchaguzi".
Ofisi yetu inapatikana barabara ya Njombe-Songea mtaa wa Mjimwema.
Sanduku la Posta: S.L.P 577
Simu ya Mezani: 026-2968833
Simu ya Mkononi: 026-2968833
Barua Pepe: td@njombetc.go.tz
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Njombe